Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uingereza, Gareth Southgate amesema mchezaji Raheem Sterling amewaomba radhi wachezaji wenzake kwa kuchelewa kuripoti kambi ya timu ya Taifa kujiandaa na kombe la dunia.
Mshambuliaji huyo wa Manchester City alipaswa kuripoti kambini Jumanne lakini amechelewa baada ya kuchanganya ndege kutoka Jamaica kurejea Uingereza.
Sterling alipamba vichwa vya habari mbalimbali Ulaya wiki hii baada ya kupiga picha akiwa amejichora tattoo yenye bastola katika mguu wake wa kulia.
Southgate yupo tayari kumtumia Sterling katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Nigeria utakaopigwa katika uwanja wa Wembley usiku wa leo.
"Aliomba radhi kwa wachezaji wenzake, ameelezea jinsi anavyoyapa umuhimu mashindano haya.
"Kila mtu amekubaliana nae baada ya mjadala mrefu, kwa sasa akili zetu tumeziamishia kwenye mashindano ya kombe la dunia," alisema Southgate.
Sterling anatarajiwa kuwa mmoja wa wachezaji muhimu wa Uingereza kwenye mashindano hayo ambapo Southgate hakuweka wazi kuwa mshambuliaji huyo amepewa adhabu gani.
About Author

Advertisement

Related Posts
- KANE AJIFUNGA ZAIDI SPURS08 Jun 20180
Nahodha wa Uingereza, Harry Kane ameongeza mkataba mrefu na timu yake ya Tottenham Hotspur iliyo...Read more »
- RIVALDO: MAN UNITED IMELAMBA DUME KWA FRED06 Jun 20180
Gwiji wa timu ya taifa ya Brazil, Rivaldo amesema Manchester United wamepata mchezaji mzuri baada ...Read more »
- BALLACK ASHANGAZWA NA SANE KUTEMWA UJERUMANI05 Jun 20180
Kiungo wa zamani wa Ujerumani Michael Ballack ameshangazwa na na kutemwa kwa winga Leroy Sane kati...Read more »
- CHELSEA YAHAMIA KWA BLANC KUCHUKUA MIKOBA YA CONTE30 May 20180
Chelsea ipo kwenye mazungumzo na kocha wa zamani wa Paris Saint-Germain na timu ya taifa ya Ufaran...Read more »
- NEYMAR AKIRI HAYUPO FITI ASILIMIA MIA28 May 20180
Zikiwa zimesalia wiki tatu kabla ya kuanza michuano ya kombe la dunia nyota wa PSG na timu ya taif...Read more »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.