Kiungo wa zamani wa Ujerumani Michael Ballack ameshangazwa na na kutemwa kwa winga Leroy Sane katika kikosi kitakacho shiriki fainali za kombe la dunia.
Sane 22, hakujumuisha na kocha Joachim Low katika kikosi cha wachezaji 23 kitacho kwenda Urusi kwa ajili ya fainali hizo.
Kiungo huyo wa zamani wa timu za Chelsea na Bayern Munich ametumia mitandao ya kijamii kuonyesha kutopendazwa na kuachwa kwa mchezaji huyo bora kijana wa mwaka wa ligi kuu nchini Uingereza.
"Ujerumani ya Low inataka kujiweka kwenye presha, Sane ni mchezaji bora kijana wa ligi kuu Uingereza unaweza kumuacha nyumbani katika mashindano haya makubwa," aliandika Ballack kupitia mtandao wa Twitter.
Winga huyo wa Manchester City hajaifungia Ujerumani bao lolote katika michezo 12 aliyocheza kwenye timu ya wakubwa lakini msimu huu amefungia klabu yake mabao 10 na kusaidia mengine 15.
About Author

Advertisement

Related Posts
- KANE AJIFUNGA ZAIDI SPURS08 Jun 20180
Nahodha wa Uingereza, Harry Kane ameongeza mkataba mrefu na timu yake ya Tottenham Hotspur iliyo...Read more »
- RIVALDO: MAN UNITED IMELAMBA DUME KWA FRED06 Jun 20180
Gwiji wa timu ya taifa ya Brazil, Rivaldo amesema Manchester United wamepata mchezaji mzuri baada ...Read more »
- STEALING AOMBA RADHI KWA KUCHELEWA KURIPOTI 'THREE LIONS'02 Jun 20180
Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uingereza, Gareth Southgate amesema mchezaji Raheem Sterling amewao...Read more »
- CHELSEA YAHAMIA KWA BLANC KUCHUKUA MIKOBA YA CONTE30 May 20180
Chelsea ipo kwenye mazungumzo na kocha wa zamani wa Paris Saint-Germain na timu ya taifa ya Ufaran...Read more »
- NEYMAR AKIRI HAYUPO FITI ASILIMIA MIA28 May 20180
Zikiwa zimesalia wiki tatu kabla ya kuanza michuano ya kombe la dunia nyota wa PSG na timu ya taif...Read more »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.