Miamba ya soka nchini timu za Simba na Yanga zimepangwa kundi moja katika michuano ya Cecafa Kagame Cup itakayoanza Juni 29 mpaka Julai 13 jijini Dar es Salaam.
Timu hizo zimepangwa kundi C pamoja na timu za St. George ya Ethiopia na Dakadaha ya Somalia.
Katibu mkuu wa Cecafa, Nicholas Musonye amesema wanaamini michuano itakuwa mizuri kutokana Tanzania kuwa na historia nzuri kila inapoandaa.
"Michuano ya Cecafa itaanza Juni 28 mpaka Julai 13 na itashirikisha timu 12 kutoka katika ukanda wetu huu wa Afrika Mashariki na Kati," alisema Musonye.
Michuano hiyo itarushwa moja kwa moja na Azam TV ambapo Mkurugenzi wake Tido Muhando amesema wamejipanga vizuri kuhakikisha inakuwa bora na ya kuvutia.
Katika michuano hiyo mabingwa watetezi Azam FC imepangwa kundi A pamoja na JKU ya Zanzibar, Uganda Reps ya Uganda pamoja na Kator FC ya Sudan Kusini.
Kundi B itakuwa na timu za Rayon Sports ya Rwanda, Gor Mahia ya Kenya, Lydia Ludic ya Burundi pamoja na Ports ya Djibouti.
Michuano itachezwa katika viwanja viwili ambavyo ni Azam Complex na Uwanja wa Taifa.
SIMBA, YANGA USO KWA USO KAGAME CUP
Title: SIMBA, YANGA USO KWA USO KAGAME CUP
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Miamba ya soka nchini timu za Simba na Yanga zimepangwa kundi moja katika michuano ya Cecafa Kagame Cup itakayoanza Juni 29 mpaka Julai 13...
Post a Comment