Nahodha wa Uingereza, Harry Kane ameongeza mkataba mrefu na timu yake ya Tottenham Hotspur iliyomlea tangu akiwa mtoto.
Kane amesaini mkataba wa miaka sita utakaomuweka klabuni hapo mpaka 2024.
Kane ni miongoni mwa washambuliaji bora kwa sasa duniani ambapo amefunga mabao 41 katika michezo 48 aliyocheza msimu huu.
Mkataba huo unamaanisha Kane 24, atakuwepo katika uwanja wao mpya wa London katika msimu wa 2018/19.
Post a Comment