Mlinda mlango wa timu ya Simba, Aishi Manula ameshangazwa na waamuzi wa Kenya kumzuia kuweka taula lake golini kwenye hatua za penati wakati katika muda wa kawaida wanamruhusu kufanya hivyo.
Katika mchezo wa jana wa nusu fainali ya kwanza ya michuano ya SportPesa Super Cup dhidi ya KK Homeboyz, Manula alizuiwa kuweka taulo hilo golini na waamuzi kitu ambacho kilimshangaza.
Manula aliyasema hayo baada ya kumaliza kipindi cha mazoezi asubuhi huku akisema wanalihusisha na imani za kishirikina.
Mwaka 2013 mlinda mlango mwingine wa Tanzania, Ivo Mapunda alijipatia umaarufu akiwa na timu ya Gor Mahia kupitia taulo alilokuwa akiliweka golini kutokana na uwezo mkubwa wa kudaka penati kila akiligusa.
"Nawashangaa hawa marefa wananikataza kuweka taulo langu golini wakati wa penati tu lakini dakika 90 hawalizuii, nadhani wanahisi kuna mambo ya kishirikina kitu ambacho sio cha kweli," alisema Manula.
Manula anategemewa kuwa golini katika mchezo wa fainali siku ya Jumapili dhidi ya Gor Mahia.
About Author
The part time Blogger love to blog on various categories like Web Development, SEO Guide, Tips and Tricks, Android Stuff, etc including Linux Hacking Tricks and tips. A Blogger Template Designer; designed many popular themes.
Advertisement
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment