Zikiwa zimesalia wiki tatu kabla ya kuanza michuano ya kombe la dunia nyota wa PSG na timu ya taifa Brazil, Neymar amekiri kuwa hayupo fiti asilimia 100.
Mshambuliaji huyo amerejea mazoezini baada ya kutoka kufanyiwa upasuaji wa goti mwezi Februari.
Neymar anatarajia kuiongoza Brazil katika mechi ya kirafiki dhidi ya Croatia Junei 3, ingawa amesema bado hajapona vizuri.
"Bado sijapona kwa asilimia 100, hii itanichukua muda kidogo kurejea kabisa, wakati mwingine nakosa ila kujiamini ninapokimbia na mpira uwanjani ila haitachukua muda nitakuwa nimerejea moja kwa moja," alisema Neymar.
Brazil itacheza mechi yake ya ufunguzi ya michuano ya kombe la dunia dhidi ya Uswisi Juni 17.
NEYMAR AKIRI HAYUPO FITI ASILIMIA MIA
Title: NEYMAR AKIRI HAYUPO FITI ASILIMIA MIA
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Zikiwa zimesalia wiki tatu kabla ya kuanza michuano ya kombe la dunia nyota wa PSG na timu ya taifa Brazil, Neymar amekiri kuwa hayupo fit...
Post a Comment