Gor Mahia imetawazwa mabingwa wa SportPesa Super Cup kwa mara ya pili mfululizo baada ya kuifunga Simba mabao 2-0 katika mchezo wa fainali uliofanyika katika uwanja wa Afraha.
Gor imemaliza michuano ikiwa haijaruhusu nyavu zake kuguswa hata mara moja huku wakifunga mabao saba.
Mshambuliaji Maddie Kagere aliifungia Gor bao la mapema dakika ya sita baada ya kupokea safi ya Jacques Tuyisenge.
Kagere ameibuka mfungaji bora wa michuano hiyo kwa mara pili mfululizo baada ya kufunga mabao manne.
Baada ya bao hilo Simba ilifanya mashambulizi kadhaa lakini walikosa muunguniko kutoka idara ya kiungo kwenda kwa washambuliaji huku wakipoteza sana mipira.
Tuisenge aliifungia Gor bao la pili kwa dakika ya 55 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na kiungo Humphrey Mieno.
Pamoja na taji na pesa taslimu Gor watakwenda Uingereza kucheza na Everton katika uwanja Goodison Park.
hakika
ReplyDeletesana
Awesome! ATZ Sport is my top choice for watching live sports online. Can't wait for the next match!
ReplyDelete