Kocha wa Singida United, Hans van Pluijm ameweka wazi kuwa atafurahi kama awaachia ubingwa wa FA 'Walima alizeti' hao katika mchezo wa fainali dhidi ya Mtibwa Sugar jioni ya leo.
Fainali hiyo itachezwa katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha saa 9 alasiri huku wadau wengi wakiendelea kumimimika jijini humo kutoka sehemu mbalimbali kuitazama.
Mchezo huo ni wa mwisho kwa Pluijm kuiongoza Singida kwakua tayari amejiunga na klabu ya Azam FC na baada ya mechi kumalizika ataondoka na viongozi wa matajiri hao kurejea Dar es Salaam.
Mholanzi huyo amesema akichukua ubingwa itakuwa ni historia kubwa kwake na klabu pia lakini kwakua anaondoka itakuwa amewaachia zawadi nzuri.
Hata hivyo Pluijm amekiri kuwa hana uhakika wa kufanikisha jambo hilo kwakua Mtibwa ni timu nzuri na ina wachezaji bora hivyo itabidi wapambane ili kukamilisha azma hiyo.
"Ubingwa siku zote ni historia nzuri kwa wachezaji na klabu lakini kwakua sitakuwa na Singida msimu ujao nitafurahi kama nitawapa ubingwa wa FA," alisema Pluijm.
About Author

Advertisement

Related Posts
- GOR MAHIA YATETEA UBINGWA WA SPORTPESA10 Jun 20182
Gor Mahia imetawazwa mabingwa wa SportPesa Super Cup kwa mara ya pili mfululizo baada ya kuifu...Read more »
- SINGIDA MSHINDI WA TATU SPORTPESA10 Jun 20180
Singida United imekuwa mshindi wa tatu katika michuano ya SportPesa Super Cup baada ya kuifunga Ka...Read more »
- KIKOSI CHA SIMBA DHIDI YA GOR MAHIA10 Jun 20182
1. Aishi Manula 2. Shomari Kapombe 3. Paul Bukaba 4. Yusuf Mlipili 5. Eraston nyoni (c) 6. Jonas M...Read more »
- MASOUD: TUTAKUJA KIVINGINE KESHO WATU HAWATAAMINI09 Jun 20180
Kaimu kocha mkuu wa timu ya Simba, Masoud Djuma amesema katika mchezo wa kesho wa fainali dhidi ya...Read more »
- TAARIFA YA DAKTARI JUU YA JERAHA LA NGOMA09 Jun 20180
Daktari wa timu ya Azam, Mwanandi Mwankemwa amethibitisha kuwa mshambuliaji Donald Ngoma atakuwa n...Read more »
- SIMBA: TUNAIHESHIMU GOR LAKINI HATUIOGOPI09 Jun 20180
Uongozi wa klabu ya Simba umekiri kuwa mchezo wa kesho wa fainali ya SportPesa Super Cup dhidi ya ...Read more »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
amulVsorpre Jill Smith link
ReplyDeletesaufunctratop