Mtibwa Sugar ndio mabingwa wapya wa kombe la Azam Sports Federation Cup baada ya kupata ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Singida United katika mchezo wa fainali uliofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
Singida walicheza vizuri katika mchezo huo wakati Mtibwa ikionekana kutafuta matokeo na ambayo walifanikiwa kuyapata.
Mtibwa ilipata mabao mawili kipindi cha Kwanzaa dakika za 21 na 37 kupitia kwa Salum Kihimbwa na Issa Rashid 'Baba Ubaya'.
Salum Chuku aliifungia Singida bao la kwanza dakika ya 43 kabla ya Tafadzwa Kutinyu kuongeza la pili dakika ya 69.
Mwamuzi Emmanuel Mwandembwa alimtoa nje Baba Ubaya kwa kadi nyekundu kufuatia kadi ya pili ya njano dakika ya 80.
Ismail Mhesa aliifungia Mtibwa bao la ushindi dakika ya 88 baada ya kupokea pasi safi ya Kelvin Sabato.
About Author

Advertisement

Related Posts
- GOR MAHIA YATETEA UBINGWA WA SPORTPESA10 Jun 20182
Gor Mahia imetawazwa mabingwa wa SportPesa Super Cup kwa mara ya pili mfululizo baada ya kuifu...Read more »
- SINGIDA MSHINDI WA TATU SPORTPESA10 Jun 20180
Singida United imekuwa mshindi wa tatu katika michuano ya SportPesa Super Cup baada ya kuifunga Ka...Read more »
- KIKOSI CHA SIMBA DHIDI YA GOR MAHIA10 Jun 20182
1. Aishi Manula 2. Shomari Kapombe 3. Paul Bukaba 4. Yusuf Mlipili 5. Eraston nyoni (c) 6. Jonas M...Read more »
- MASOUD: TUTAKUJA KIVINGINE KESHO WATU HAWATAAMINI09 Jun 20180
Kaimu kocha mkuu wa timu ya Simba, Masoud Djuma amesema katika mchezo wa kesho wa fainali dhidi ya...Read more »
- TAARIFA YA DAKTARI JUU YA JERAHA LA NGOMA09 Jun 20180
Daktari wa timu ya Azam, Mwanandi Mwankemwa amethibitisha kuwa mshambuliaji Donald Ngoma atakuwa n...Read more »
- SIMBA: TUNAIHESHIMU GOR LAKINI HATUIOGOPI09 Jun 20180
Uongozi wa klabu ya Simba umekiri kuwa mchezo wa kesho wa fainali ya SportPesa Super Cup dhidi ya ...Read more »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.