Rais wa klabu ya Simba Evans Aveva amesema Simba wanaenda
kuishtaki TFF, FIFA katika mahakama ya usuluhishi. Akizungumza na waadishi wa
habari amesema kuwa sababu zilizotolewa na Kamati ya Katiba Sheria na Hadhi za
Wachezaji hazikuwa na mashiko kwani suala la mchezaji kucheza akiwa na kadi
tatu ni kosa kwa mujibu wa kanuni.
Aveva amesema Simba ina subiri kupewa barua na (TFF)
inayo onyesha kupokwa pointi hizo ili kuweza kupeleka malalamiko yao katika
mahakama ya usuluhishi
Simba imekuwa ikionewa na TFF kutokana na maamuzi
mbalimbali yanayotolewa ndiyo maana wakaamua kupeleka malalamiko yao FIFA
amesema Rais wa Simba.
Mapema mwezi April Kamati ya Katiba Sheria na hadhi
za Wachezaji ili pindua matokeo ya Kamati ya usimamizi na undeshwaji wa ligi
(Kamati ya saa 72) iliyoipa Simba pointi tatu kufuatia timu ya Kagera Sugar
kumchezesha beki Mohammed Fakhi aliyekuwa na kadi tatu za njano.
Walete barua twende mbele,kama haki yetu itapatikana tu
ReplyDeleteKazi ipo.
ReplyDeleteNina wasiwasi hiyo barua inaweza kutolewa ligi ikiwa imeshaisha
ReplyDeleteHUKO NDIO TUTAELEWANA VIZURI SASA.
ReplyDelete