SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: SIMBA YAIPELEKA TFF, FIFA AVEVA
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Rais wa klabu ya Simba Evans Aveva amesema Simba wanaenda kuishtaki TFF, FIFA katika mahakama ya usuluhishi. Akizungumza na waadishi wa h...
Rais wa klabu ya Simba Evans Aveva amesema Simba wanaenda kuishtaki TFF, FIFA katika mahakama ya usuluhishi. Akizungumza na waadishi wa habari amesema kuwa sababu zilizotolewa na Kamati ya Katiba Sheria na Hadhi za Wachezaji hazikuwa na mashiko kwani suala la mchezaji kucheza akiwa na kadi tatu ni kosa kwa mujibu wa kanuni.

Aveva amesema Simba ina subiri kupewa barua na (TFF) inayo onyesha kupokwa pointi hizo ili kuweza kupeleka malalamiko yao katika mahakama ya usuluhishi

Simba imekuwa ikionewa na TFF kutokana na maamuzi mbalimbali yanayotolewa ndiyo maana wakaamua kupeleka malalamiko yao FIFA amesema Rais wa Simba.

Mapema mwezi April Kamati ya Katiba Sheria na hadhi za Wachezaji ili pindua matokeo ya Kamati ya usimamizi na undeshwaji wa ligi (Kamati ya saa 72) iliyoipa Simba pointi tatu kufuatia timu ya Kagera Sugar kumchezesha beki Mohammed Fakhi aliyekuwa na kadi tatu za njano.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top