SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: DANI ALVES AIKATALIA BARCELONA
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Ilidhaniwa kwamba maajabu ya soka yangeweza kuifanya Barcelona ipindue tena matokeo ya mechi ya mkondo wa awali dhidi ya juventus kam...


Ilidhaniwa kwamba maajabu ya soka yangeweza kuifanya Barcelona ipindue tena matokeo ya mechi ya mkondo wa awali dhidi ya juventus kama walivyofanya dhidi ya PSG kwenye hatua ya 16 bora pale walipogeuza kipigo cha magoli 4 kwa 0 na kushinda Goli 6 mechi ya marudiano,lakini Jana haikuwa hivyo pale mchezaji wao wa zamani na aliyepata mafanikio makubwa na timu hiyo Dani alves alipowaongoza wachezaji wenzake wa juventus na kufanikiwa kupata suluhu katika mchezo wa pili wa robo fainali wa ligi ya mabingwa wa ulaya na kufanikiwa kuingia nusu fainali.

Barcelona walikuwa wanajipa matumaini ya kupindua matokeo lakini walikuwa juventus ndio walianza kutengeneza nafasi mbili za wazi katika dakika za mwanzo kupitia kwa mshambuliaji wake raia wa Argentina Gonzalo higuian lakini alikosa umakini wa kumalizia,Barcelona ilijitahidi kupigana na kushambulia kupitia kwa Messi na Neymar Jnr lakini ukuta imara wa waitaliano hao uliweza kuzuia kila shambulio lililopelekwa kwao hivyo kupelekea dakika 90 kumalizika kwa Barcelona 0 Juventus 0 na kufanya matokeo ya jumla yabaki 3-0.

Kwa matokeo hayo juventus inaungana na Monaco waliowafumua Dortmund kwa goli 3-1 katika mechi nyingine ilofanyika Jana usiku,pamoja na Atletico Madrid na Real Madrid zote za Hispania.
Droo ya mechi za nusu fainali na fainali.zitafanyika kesho huko katika mji wa Nyon nchini uswis na Fainali inatarajia kufanyika.June 3,2017 katika uwanja wa Taifa wa wales huko katika mji wa Cardiff.


About Author

Advertisement

Post a Comment

  1. Walijua hawa ni wafaransa,dadeki wamekutana na ukuta wa berlin

    ReplyDelete

 
Top