Ilidhaniwa kwamba maajabu ya soka yangeweza kuifanya
Barcelona ipindue tena matokeo ya mechi ya mkondo wa awali dhidi ya juventus
kama walivyofanya dhidi ya PSG kwenye hatua ya 16 bora pale walipogeuza kipigo
cha magoli 4 kwa 0 na kushinda Goli 6 mechi ya marudiano,lakini Jana haikuwa
hivyo pale mchezaji wao wa zamani na aliyepata mafanikio makubwa na timu hiyo
Dani alves alipowaongoza wachezaji wenzake wa juventus na kufanikiwa kupata
suluhu katika mchezo wa pili wa robo fainali wa ligi ya mabingwa wa ulaya na
kufanikiwa kuingia nusu fainali.
Barcelona walikuwa wanajipa matumaini ya kupindua
matokeo lakini walikuwa juventus ndio walianza kutengeneza nafasi mbili za wazi
katika dakika za mwanzo kupitia kwa mshambuliaji wake raia wa Argentina Gonzalo
higuian lakini alikosa umakini wa kumalizia,Barcelona ilijitahidi kupigana na
kushambulia kupitia kwa Messi na Neymar Jnr lakini ukuta imara wa waitaliano
hao uliweza kuzuia kila shambulio lililopelekwa kwao hivyo kupelekea dakika 90
kumalizika kwa Barcelona 0 Juventus 0 na kufanya matokeo ya jumla yabaki 3-0.
Kwa matokeo hayo juventus inaungana na Monaco
waliowafumua Dortmund kwa goli 3-1 katika mechi nyingine ilofanyika Jana
usiku,pamoja na Atletico Madrid na Real Madrid zote za Hispania.





Walijua hawa ni wafaransa,dadeki wamekutana na ukuta wa berlin
ReplyDelete