SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: SIMBA TUNATAKA HAKI YETU ASEMA MANARA
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Wekundu wa Msimbazi Simba Sports Club wameiomba Serikali kuingili swala Kagera Sugar kupokwa pointi tatu kwa kumchezesha beki Mohammed...
Wekundu wa Msimbazi Simba Sports Club wameiomba Serikali kuingili swala Kagera Sugar kupokwa pointi tatu kwa kumchezesha beki Mohammed Fakhi ambaye alikuwa na kadi tatu za njano.

 Msemaji wa klabu hiyo Haji Manara amesema Kamati ya masaa 72 chini ya Mwenyekiti wake Hamad Yahaya iliipa Simba pointi tatu kufuatia  baada ya kujiridhisha kuwa mchezaji Fakhi alikuwa na kadi tatu za njano.

Kamati ya katiba sheria na hadhi haina mamlaka ya kupitia shauli hili kwa kuwa maamuzi yanatolewa na bodi yenyewe ya ligi na wala sio kamati hiyo wamesema Manara

Kamati ya Bodi ya Ligi chini ya Mwenyekiti wake Hamad Yahaya ilishatoa maamuzi na ilijiridhisha kuwa mchezaji Fakhi ana kadi Tatu za njano
 
Haijawahi kutokea mchezaji aliyepewa kadi anaitwa kuitwa kuhojiwa amesema Manara

Manara amesema wanawapa TFF mpaka jumatatu wawe wametoa maamuzi yote ya kesi mbalimbali wamechoka kuonewa sasa. na yupo tayari kufungiwa baada ya press yake ya leo.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top