SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: RONALDO AMFUKUZIA MESSI LIGI YA MABINGWA
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Ronaldo na mpira wake baada ya kupiga hat-trick jana Magoli matatu aliyopiga Jana usiku dhidi ya Bayern Munich kwenye mechi ya marudiano...
Ronaldo na mpira wake baada ya kupiga hat-trick jana
Magoli matatu aliyopiga Jana usiku dhidi ya Bayern Munich kwenye mechi ya marudiano ya ligi ya Mabingwa barani Ulaya, yanamfanya Christiano Ronaldo dos Santos kufikisha magoli 7 msimu huu na mabao 103 katika mechi 148 za ligi ya mabingwa barani Ulaya kwa ujumla.

Ronaldo ambaye msimu huu alionekana kupotea kwenye ufungaji kwenye mechi za ligi ya mabingwa, amefunga magoli matano katika mechi mbili za robo fainali dhidi ya Bavarians, na sasa amebakiza magoli manne ili kumfikia hasimu wake Lionel Messi mwenye magoli 11.

Ifuatayo ni orodha ya wafungaji magoli Uefa msimu huu

1.Lionel Andress Messi....11
2.Edinson Roberto Cavani....8
3.Roberto Lewandowski.....8
4.Christiano Ronaldo.........7
5. Piere Emeric Aubemayang...7
6. Antonie Griezman....5
7. Dries Martens.......5
8. Karim benzema....5
9. Sergio kun Aguero...5
10. Andre Miguel Silva...4.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top