Shirikisho la Mpira wa barani Afrika (CAF), limevipitisha Viwanja vya
Uhuru, Dar es Salaam na CCM Kirumba, jijini Mwanza kwa ajili ya
michuano mbalimbali ya kimataifa ngazi ya klabu na timu za taifa.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), linachukua nafasi hii
kuwapongeza wamiliki viwanja hivyo kwa namna walivyoweza kutunza hadi
kukidhi matakwa ya CAF.
Pongezi zinakwenda kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
ambao kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ndio
wamiliki wa Uwanja wa Uhuru na Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mwanza ambao
ndio wamiliki wa Uwanja wa CCM Kirumba.
Viwanja hivyo vilikaguliwa hivi karibuni kwa nyakati tofauti na
Mkaguzi wa CAF na FIFA, Maxwell Mtouga kwa kukagua vema na kutoa taarifa
ambayo imefanya taasisi za CAF na FIFA - zinazoongoza mpira wa miguu,
kupitisha viwanja hivyo kwa ajili ya kutumika kwa ajili ya mechi za
kimataifa.
About Author

Advertisement

Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment