Uongozi wa klabu ya Yanga umetoa sababu ya kukubali kipigo cha mabao 4-0 kutoka kwa USM Alger ni wachezaji wake kukosa uzoefu wa michuano hiyo na sio ubora kama wengi wanavyodhani.
Yanga ilikosa huduma ya wachezaji wake nyota wa tano wa kikosi cha kwanza ambao ni Kelvin Yondani, Papy Tshishimbi, Obrey Chirwa, Ibrahim Ajibu na Thaban Kamusoko.
Mwenyekiti wa kamati ya mashindano ya klabu hiyo Hussein Nyika ambaye ameambatana na timu hiyo amesema kikubwa kilichowaponza ni kukosa uzoefu.
Nyika amesema wanarejea nyumbani kujiandaa na mechi zijazo za mashindano hayo kwakua walimu wameona mapungufu yaliyojitokeza na watayafanyia kazi.
"Tumekubali kipigo cha mabao hayo kwakua wachezaji wetu walikosa uzoefu ukilinganisha na wapinzani wetu," alisema Nyika.
YANGA YASEMA HAIKUWA DHAIFU BALI ILIKOSA UZOEFU
Title: YANGA YASEMA HAIKUWA DHAIFU BALI ILIKOSA UZOEFU
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Uongozi wa klabu ya Yanga umetoa sababu ya kukubali kipigo cha mabao 4-0 kutoka kwa USM Alger ni wachezaji wake kukosa uzoefu wa michuano...
Post a Comment