Klabu ya Yanga imelitaka Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) kuacha kuwakata pesa kulipa deni wanalodaiwa kwakua wapo katika kipindi kigumu kiuchumi.
TFF imekuwa ikizuia mapato ya Yanga ya uwanjani na kutoka vyanzo yanayopitia kwake ili kufidia deni wanalowadai.
Mwaka 2016 aliyekuwa Mwenyekiti wa klabu hiyo, Yusuph Manji aliruhusu mashabiki kuingia bure katika mchezo wa klabu bingwa Afrika dhidi ya TP Mazembe lakini hakulipa gharama za mechi.
Mwenyekiti wa matawi ya Yanga, Bakili Makele amewataka TFF ikate pesa katika deni wanalolidai Shirikisho hilo zaidi ya sh milioni 200 lakini sio kuzuia mapato yao ya uwanjani kipindi hiki.
"Kama TFF au Bodi ya ligi inatudai chochote ikate kwenye hela tunayowadai lakini sio kuzuia mapato yetu kwa sasa tupo kwenye hali ngumu.
"Sio siri kwa sasa tumeyumba kichumi na tuna hali mbaya kwahiyo TFF iache kuzuia mapato yetu ya uwanjani," alisema Bakili.
Post a Comment