Timu ya Yanga ina nafasi ya kumaliza nafasi ya pili juu ya Azam kama itaibuka na ushindi katika mechi baina yao itakayopigwa katika uwanja wa Taifa saa mbili usiku wa leo.
Yanga ipo nyuma ya Azam kwa pointi tatu na kama itashinda mchezo wa leo watakuwa sawa kwa alama lakini vijana hao wa Jangwani watakuwa na uwiano mzuri wa mabao ya kufunga.
Yanga haikuwa na mwenendo mzuri msimu huu hasa katika mzunguko wa pili baada ya kupoteza mechi nyingi huku ikipoteza nne mfululizo wakati Azam ikifanya vizuri zaidi mzunguko wa pili.
Kuelekea mchezo huo Azam iliweka wazi kuwa wataingia kwa tahadhari kubwa wakiwapa heshima Yanga huku wakiahidi kushusha kikosi kizima kwenye mtanange huo.
"Tunaiheshimu Yanga, haikuwa na msimu mzuri lakini haitupi uhakika wa kuibuka na ushindi kikubwa tumejipanga vizuri," alisema Msemaji wa Azam, Jaffer Idd.
Kwa upande wake mjumbe wa kamati ya mashindano, Hussein Nyika amesema wameuchukuli mchezo huo kwa umuhimu mkubwa huku wachezaji wao wakiwa katika hali nzuri.
Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza uliofanyika katika uwanja wa Azam Complex, Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-1.
Mabingwa hao wa zamani hawapewi nafasi kubwa ya kufanya vizuri kwenye mchezo wa leo lakini swali Je Yanga itapindua meza kibabe kumaliza ligi juu ya Azam?
YANGA KUPINDUA MEZA KIBABE MBELE YA AZAM LEO?
Title: YANGA KUPINDUA MEZA KIBABE MBELE YA AZAM LEO?
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Timu ya Yanga ina nafasi ya kumaliza nafasi ya pili juu ya Azam kama itaibuka na ushindi katika mechi baina yao itakayopigwa katika uwanja...
Post a Comment