Uongozi wa klabu ya Simba umetaja sababu ya kuacha baadhi ya wachezaji katika mchezo wa mwisho wa ligi dhidi ya Majimaji leo jioni kuwa michuano ya SportPesa Super Cup.
Simba itashiriki michuano hiyo itakayoanza Juni 3 nchini Kenya ambayo itakuwa na timu nane kutoka Tanzania na Kenya.
Msemaji wa klabu ya Simba, Hajji Manara amesema maamuzi hayo yametokana na ushauri wa benchi la ufundi kuwa katika mchezo huo watumike wachezaji ambao hawakupata nafasi kubwa ya kucheza msimu huu wengine wakijiandaa na michuano hiyo.
Manara aliongeza kuwa wamepanga kuhakikisha wanafanya vizuri kwenye michuano hiyo ili kupata nafasi ya kucheza na Everton katika uwanja wa Godson Park kama watawaa ubingwa.
"Tumekigawa kikosi chetu, wengine wameenda Songea kwa ajili ya mechi ya leo dhidi ya Majimaji wengine wamebaki kujiandaa na michuano ya SportPesa.
"Tumejipanga kuhakikisha tunafanya vizuri katika michuano hiyo na tutapeleka kikosi kizima ndio maana tuwapumzisha baadhi ya wachezaji," alisema Manara.
Baadhi ya nyota wa Simba ambao hawajasafiri na timu hiyo ni John Bocco, Emmanuel Okwi, Aishi Manula, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni na Shiza Kichuya.
SIMBA YATAJA SABABU YA KUWAACHA BAADHI YA NYOTA WAKE
Title: SIMBA YATAJA SABABU YA KUWAACHA BAADHI YA NYOTA WAKE
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Uongozi wa klabu ya Simba umetaja sababu ya kuacha baadhi ya wachezaji katika mchezo wa mwisho wa ligi dhidi ya Majimaji leo jioni kuwa mi...
Post a Comment