Chama cha soka nchini Misri (EFA) kimetoa taarifa kuwa mshambuliaji Mohamed Salah hajaumia sana kama ilivyotegemewa awali.
Nyota huyo wa Liverpool alitolewa nje nusu saa baada ya kuanza mechi ya fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya walipokubali kipigo cha mabao 3-1 kutoa kwa Real Madrid baada ya kuumizwa bega na Sergio Ramos.
Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp alisema mshambuliaji huyo alipata maumivu makubwa ingawa anasubiri vipimo ili kufahamu kama ataweza kushiriki fainali za kombe la dunia mwezi ujao.
Kupitia mtandao wa Tweeter, EFA imesema imewasiliana na madaktari wa Liverpool na kuthibitisha kuwa vipimo vya x-ray alivyofanyiwa vimeonyesha kuwa Salah hajaumia sana.
Chama hicho kimeongeza kuwa Salah anatarajia kuwa fiti katika mchezo wa kwanza wa Misri wa kundi A wa kombe la dunia dhidi ya Uruguay, Juni 15.
SOMA MAANDELEO YA HALI YA SALAH
Title: SOMA MAANDELEO YA HALI YA SALAH
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Chama cha soka nchini Misri (EFA) kimetoa taarifa kuwa mshambuliaji Mohamed Salah hajaumia sana kama ilivyotegemewa awali. Nyota huyo w...
Post a Comment