Timu ya Yanga imesema inahitaji ushindi kwa hali yoyote katika mchezo wa kesho wa kombe la Shirikisho Afrika hatua ya makundi dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda.
Mchezo huo utapigwa saa 1 jioni katika uwanja wa Taifa huku Yanga ikihitaji ushindi kufuatia kipigo cha mabao 4-0 ilichopata katika mchezo wa kwanza dhidi ya USM Alger ya Algeria.
Kaimu kocha mkuu wa Yanga, Noel Mwandila amesema kesho wataingia uwanjani wakiwa na lengo moja tu kushinda ili kufufua matumaini ya kufanya vizuri kwenye michuano hiyo.
"Tunahitaji ushindi kwa hali yoyote hata ikiwa bao moja kwakua michuano hii lazima kushinda nyumbani ili kujiweka vizuri vinginevyo hauwezi kufika mbali," alisema Mwandila.
Katika mchezo huo Yanga itawakosa Said Makapu mwenye adhabu ya kadi, Papy Tshishimbi majeruhi na Ibrahim Ajib ana matatizo ya kifamilia.
Wachezaji Obrey Chirwa, Thaban Kamusoko na Amiss Tambwe wanatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi kitakachoshuka dimbani kesho baada ya kupona majeraha.
YANGA: IWE JUA AU MVUA KESHO USHINDI MUHIMU
Title: YANGA: IWE JUA AU MVUA KESHO USHINDI MUHIMU
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Timu ya Yanga imesema inahitaji ushindi kwa hali yoyote katika mchezo wa kesho wa kombe la Shirikisho Afrika hatua ya makundi dhidi ya Ray...
Post a Comment