Simba imefanikiwa kutwaa ubingwa huo na Jumamosi Mei 19 watakabidhiwa kombe hilo kwakua ndio utakuwa mchezo wa mwisho kucheza katika uwanja wa nyumbani.
Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia amesema wamemuandikia barua Waziri wa Michezo Dk. Harrison Mwakyembe kumuarifu Rais Magufuli kwa ajili ya kujitokeza katika hafla hiyo.
Rais wa TFF Wallace Karia |
Kabla ya kuwakabidhi Simba taji hilo la ubingwa Rais Magufuli atakabidhiwa kombe la CECAFA la vijana wa timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17 'Serengeti Boys' walilotwaa nchini Burundi.
Mchezo huo unatarajiwa kuanza saa 8 mchana ili kutoa nafasi kwa matukio hayo kufanyika huku kiingilio cha chini kikiwa shilingi elfu tatu.
Ratiba ya Mh.isipobadilika akafanikiwa kuja Taifa na tukakabidhiwa ndoo na mzee wa kutumbua naamini upande wa pili itawauma sana.....na wanaomba usiku mchana isiwe hahaaaaaa SIMBA TAIFA KUBWA
ReplyDeleteDaaah! Hiyo siku si mchezo ni bab kubwa,Mungu amjalie Mzee baba Anko Magu atimbe Taifa kuwakabidhi machampion wa ukweli kombe letu,THIS IS SIMBA braza
ReplyDeleteKila utawala na zama zake bwana
ReplyDelete