SportPesa ndio wadhamini wakuu wa mabingwa hao ambapo kwa mujibu wa mkataba wao kila inapotwaa ubingwa wanapata kiasi hicho cha pesa.
Kikosi cha mabingwa hao wakiwa na benchi lao la ufundi wamepeleka kombe la ubingwa katika ofisi za SportPesa zilizopo Masaki jijini Dar es Salaam.
Hundi hiyo ilikabidhiwa na Mkurugenzi wa SportPesa Tanzania, Tarimba Abbas iliyopokelewa na Kaimu Makamu wa Rais wa Simba, Iddi Kajuna na Nahodha wa timu hiyo John Bocco
Baada ya ligi kuu kumalizika Jumatatu wiki ijayo Wekundu hao wataelekea nchini Kenya kushiriki michuano ya SportPesa Super Cup itakayoanza Juni 5.
Michuano hiyo itashirikisha timu nane, nne kutoka Tanzania ambazo ni Simba, Yanga, Singida United na JKU wakati nyingine ni Gor Mahia, Nakuru All Stars, AFC Leopards kutoka Kenya.
This comment has been removed by the author.
ReplyDeleteswafiiiii
ReplyDeleteHizo pesa za ubingwa wa Sportpesa super Cup watupe tu mapemaaaa.....maana tunaenda kubeba
ReplyDelete