SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: MO AKUBALI ASILIMIA 49 SIMBA
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Mfanyabiashara Mohammed Dewji 'MO' amekubali kuwekeza kwa asilimia 49 katika klabu ya Simba kama ilivyoelekezwa na Serikali. Awa...
Mfanyabiashara Mohammed Dewji 'MO' amekubali kuwekeza kwa asilimia 49 katika klabu ya Simba kama ilivyoelekezwa na Serikali.

Awali MO alitaka kuwekeza asilimia 51 lakini ikawa 50 kabla ya Serikali kuelekeza kuwa klabu inayohitaji kubadili mfumo wa uendesheshaji kutoka umiliki wa wachamana kwenda kwenye hisa mwekezaji anatakiwa kuwekeza asilimia 49.

Baada ya kuonekana mchakato huo unachelewa ilisemekana kuwa MO aliamua kujitoa kwakua hakupenda kupewa asilimia 49 aliihitaji asilimia 50.

Mkuu wa kitengo cha habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba, Hajji Manara amewaambia Waandishi wa habari kuwa tayari MO amekubali na kila kitu kimekaa sawa.

"Niwatoe hofu wapenzi na Wanachama wa Simba kuwa MO amekubali kuwekeza kwa asilimia 49 kama maelekezo ya Serikali ilivyoagiza," alisema Manara.

Simba itafanya mkutano wao mkuu wa dharura wa wanachama siku ya Jumapili katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere kwa ajili ya kubadili katiba ya klabu hiyo ili kuendana na mfumo huo mpya wa hisa.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top