SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: HONGERENI SIMBA, MLIJIFUNZA KUTOKANA NA MAKOSA
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Alhamisi wiki iliyopita ilikuwa siku ya furaha kubwa kwa mashabiki na wapenzi wa timu ya Simba baada ya kutangaza ubingwa wa ligi kuu Tanz...
Alhamisi wiki iliyopita ilikuwa siku ya furaha kubwa kwa mashabiki na wapenzi wa timu ya Simba baada ya kutangaza ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara wakiwa wamelala majumbani mwao.

Hii ilitokana na waliokuwa mabingwa watetezi na wapinzani wao wa karibu kwenye mbio za ubingwa timu ya Yanga kukubali kipigo cha mabao 2-0 na Prisons ya mbeya.

Ni miaka 6 imepita toka Simba ilipotwaa ubingwa kwa mara ya mwisho ambapo ilikuwa ni msimu wa 2011/2012.

SDF Sports Media inakuletea sababu tano za msingi za timu hiyo kutwaa ubingwa kabla ya ligi kumalizika na bila kupoteza hata mchezo mmoja wakiwa wamebakiwa na mechi mbili.

1. Usajili bora na upana wa kikosi.

Moja kati ya matatizo makubwa ambayo Simba ilikuwa inakumbana nayo ni usajili wa kuunga unga waliokuwa wanaufanya, Simba ilishindwa kupambana na Yanga na Azam FC kwenye usajili kiasi wachezaji wengi wazuri wanasajiliwa na wapinzani wao.

Lakini kuanzia msimu ulopita na msimu huu Simba ilifanikiwa kusajili wachezaji wazuri na wenye uzoefu mkubwa usajili wa Shiza Kichuya, Mzamiru Yassin, Mohammed Ibrahim na James Kotei msimu uliongeza nguvu kubwa kikosini.

Msimu huu wamewasajili John Bocco, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, Aishi Manula, Haruna Niyonzima, Asante Kwasi, Nicholas Gyan na kurejea kwa Emmanuel Okwi uliifanya Simba kuwa imara karibia  kila idara.

2. Utulivu wa Uongozi

Pamoja na kuwa viongozi wawili wakuu Rais Evans Aveva na Makamu wake Godfrey Nyange kukabiliwa na kesi mahakamani lakini viongozi waliobaki wakiongozwa na kaimu Rais Salim  Abdallah (Try again) waliendelea kusimama imara kuhakikisha timu inapigania ubingwa ambao umepatikana.

3. Uwepo wa Mwekezaji Mohammed Dewji (MO)

Hapana shaka Mohammed Dewji amechangia kwa kiasi kikubwa mafanikio ya Simba msimu huu, kuhusika kwake kwenye usajili wa baadhi ya nyota wa timu hiyo pamoja na hamasa ya fedha alizokuwa akiitoa uliifanya Simba ipate ushindi kwenye mechi zake nyingi msimu huu.

4. Hamasa ya Mashabiki.

Mashabiki wa Simba msimu huu wamechangia sana mafanikio ya timu yao, bila kupepesa macho mechi za Simba zilikuwa zinajaza kuliko zote ndani ya Dar es Salaam au mikoani. Hamasa hiyo pia ilichangiwa na namna msemaji wa timu hiyo Hajji Manara aliyekuwa akitoa hamasa iliyowachagiza wachezaji kufanya vizuri uwanjani.
Msemaji wa Simba Hajji Manara

5.Mabadiliko ya benchi la ufundi.

Hakuna shaka mabadiliko yaliyofanywa na Uongozi kwa kumuondoa aliyekuwa kocha mkuu Joseph Omog na kumleta mrundi Masoud Djuma na badae Mfaransa Pierre Lechantre yaliisaidia sana Simba kufanya vizuri msimu huu.

Kipindi cha Omog Simba ilionekana kupata ushindi lakini wa wasiwasi, Mcameroon huyo alionekana kushindwa kuwatumia wachezaji aliyokuwa nao kiasi cha wengine kuonekana ni mzigo lakini ujio wa Masoud uliwarudisha kwenye viwango baadhi ya wachezaji hao ni Said Ndemla na Gyan.

Kwa hakika misimu yote ambayo Simba ilipotea ilisababishwa na mambo mengi lakini msimu huu wamejifunza na kufanikiwa kutwaa ubingwa.

Ni wakati wao kuanza maandalizi kwa ajili ya michuano ya klabu bingwa Afrika msimu ujao pamoja na mashindano mengine.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top