Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), linatangaza
kufungua dirisha la usajili kwa wachezaji wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara,
Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili ikiwa ni ufunguzi wa msimu mpya wa
mashindano wa 2017/2018.
Dirisha hilo linafunguliwa Juni 15, mwaka huu na
litafungwa Agosti 6, mwaka huu hivyo kila timu inayoshiriki michuano tajawa
hapo juu, inaarifiwa kufuata kalenda hiyo ambayo tunaitangaza sasa.
Tahadhali, hakutakuwa na muda wa nyongeza kwa timu ambazo
hazitakamilisha usajili kama ilivyotokea msimu uliopita kwa baadhi ya timu
kushindwa kufanya kusajili kwa wakati na dirisha likafungwa.
Post a Comment