SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: MECHI ZOTE ZA MWISHO VPL KUANZA SAA 10.00 JIONI.
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), tunafahamisha kuwa mechi za mwisho za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2016/2017zi...
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), tunafahamisha kuwa mechi za mwisho za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2016/2017zitachezwa kuanzia saa 10.00 jioni bila kujali kama jua linawahi au kuchelewa kuzama.

Muda huo umepangwa ili kuhakikisha timu zote zinamaliza mechi za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara zinamalizika siku moja ya Mei 20, mwaka huu na kwa muda mmoja, ikiwa ni pamoja na kudhibiti viashiria vyo vyote vya upangaji wa matokeo.

Ni jukumu la kila kamishna kuhakikisha mechi anayosimamia inaanza katika muda ulipangwa bila kujali kama kuna mgeni rasmi au la.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top