Timu ya
taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys jana imeibuka na
ushindi wa kwanza katika Fainali za Vijana Afrika chini ya umri wa miaka 17 dhidi
ya Angola kwa bao 2-1
Ikicheza
kwenye uwanja wa L'Amitie mjini Libreville Serengeti boys walikuwa wa kwanza
kupata bao kupitia Kevin Naftal katika dakika ya 4 kabla ya Chilumbo
kusawazisha, mpaka mapumziko Tanzania 1-1 Angola
Kipindi cha
pili kilianza kwa kasi huku timu zote zikishambuliana Serengeti boys walikosa
umakini katika kumalizia mashambulizi, dakikia ya 69 Abdul Suleiman aliwainua
ma elfu ya mashabiki wa Tanzania kwa kupiga bao safi kabisa baada ya kupokea
pasi ya Mkomola
Tanzania
anaongoza kundi B pointi 4 akifuatiwa na mali mwenye point 4 pia
Karata ya
mwisho kwa Tanzania itakuwa dhidi ya Niger ili kujihakikishia nafasi katika
nusu fainali na baadae Kombe la Dunia
Post a Comment