SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: RAMOS ASEMA AMHOFII SALAH HATA CHEMBE
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Mlinzi wa kati na nahodha wa Real Madrid Sergio Ramos amesema anamheshimu mshambuliaji wa Liverpool, Mohamed Salah kutokana na uwezo lakin...
Mlinzi wa kati na nahodha wa Real Madrid Sergio Ramos amesema anamheshimu mshambuliaji wa Liverpool, Mohamed Salah kutokana na uwezo lakini haofii kukutana nae kwenye mchezo wa fainali wa ligi ya mabingwa Ulaya.

Salah ameingoza Liverpool kufika fainali ya michuano hiyo itakayofanyika Mei 26 katika mji wa Kiev nchini Ukraine.

Raia huyo wa Misri kwa sasa anafananishwa kwa uwezo na nyota Cristiano Ronaldo na msimu huu amefunga mabao 43 kwenye mashindano yote.

Ramos amesisitiza kuwa Salah yupo kwenye kiwango bora kwa sasa lakini haofii chochote kutoka kwake.

"Tumemuona Salah anachokifanya msimu huu, lakini atakuwa mmoja wa wachezaji 11 wa Liverpool tutakao pambana nao.

"Katika kipindi changu cha kucheza soka nimekutana na washambuliaji bora duniani na niliweza kuwadhibiti hata Salah nitamzuia," alisema Ramos.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top