Mshambuliaj
wa Maji Maji Songea Marcel Kaheza
amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa mwezi April wa Ligi Kuu ya Vodacom
(VPL)Tanzania Bara.
Marcel
anatwaa tuzo hiyo baada ya kuwashinda nyota wawili wa Simba Emmanuel Okwi na
John Bocco wote wa Simba katika uchambuzi uliofanywa wiki hii na Kamati ya Tuzo hizo.
Mshambuliaji
huyo alifunga mabao 7 katika mwezi April ikiwemo hatrick dhidi ya Ruvushooting
Kaheza ameiwezesha Majimaji kutoka mkiani mwa msimamo mwezi Machi hadi nafasi ya 14 sasa.
Kaheza atapewa pesa taslimu shilingi milioni moja na wadhamini wakuu wa ligi Kampuni ya Vodacom, kisimbuzi cha Azam TV kama sehemu ya zawadi ya tuzo hiyo.
Kaheza atapewa pesa taslimu shilingi milioni moja na wadhamini wakuu wa ligi Kampuni ya Vodacom, kisimbuzi cha Azam TV kama sehemu ya zawadi ya tuzo hiyo.

Post a Comment