Didier Kavumbagu sio jina geni miongoni mwa wadau wa soka nchini kutokana na kuwahi kuzichezea timu za Yanga na Azam FC kwa nyakati tofauti.
Kavumbagu alijiunga na Yanga mwaka 2012 akitokea Atletico klabu ya Burundi na kucheza kwa miaka miwili kabla ya kujiunga na Azam ambapo hakudumu sana.
SDF Sports Media ilipata nafasi ya kufanya mahojiano nae maalum kukoka katika jiji la Brussels nchini Ubelgiji ambapo ndipo anapoishi kwa sasa ambapo amefunguka mambo mengi kuhusu soka la bongo.
BONGO NOMA KWA MIBA (USHIRIKINA)
Kavumbagu amesema moja ya sababu inayofanya soka la bongo kutopiga hatua ni kutokana na wachezaji kuamini ushirikina na kurogana.
Mshambuliaji huyo amesema wachezaji wengi kutoka nje ya Tanzania wanashindwa kufanya vizuri kutokana na kupigwa misumari.
"Wakati mwingine mchezaji anashindwa kufanya vizuri kwenye ligi sio kwamba ni mbaya kuna mambo ya ushirikina sana Bongo.
STAREHE ZINAWAMALIZA WACHEZAJI WA BONGO
Kavumbagu amesema wachezaji wengi wa Bongo wanashindwa kwenda kucheza soka la kulipwa kutokana na kuendekeza starehe. Nyota huyo ameongeza kuwa wachezaji wanapenda starehe kuliko mazoezi.
Kavumbagu amemtolea mfano Mrisho Ngassa kama mchezaji anaye endekeza sana starehe kitu ambacho kimerudisha sana maendeleo yake nyuma.
"Ngassa alikuwa anabadili wanawake kila siku, anakuja kambini na picha za wanawake aliolala nao.
SOKA LA BONGO LINALIPA
Raia huyo wa Burundi amesema wachezaji wa Bongo wanalipwa vizuri mishahara. Hata yeye mwenyewe alipohama Yanga kwenda Azam alipewa kitita kikubwa cha pesa.
"Nilipokuwa natoka Yanga kwenda Azam nilipata kiasi kikubwa cha pesa, klabu za Bongo zinajitahidi sana kulipa pesa nzuri.
AMVULIA KOFIA KAPOMBE
Mshambuliaji huyo amemwagia sifa kiraka wa Simba, Shomari Kapombe kwa nidhamu aliyokuwa nayo pamoja na kujituma uwanjani.
Kavumbagu alisema "Kapombe anajitambua, anafanya mazoezi sana ndio maana hata akiwa majeruhi akirudi uwanjani anakuwa kwenye kiwango chake kile kile. Nadhani atafika mbali.
APIGA NDONDO UBELGIJI
Kwa sasa Kavumbagu anacheza soka la mtaani (Ndondo) nchini Ubelgiji huku akifanya shughuli nyingine zinazo muingizia kipato akiendelea kutafuta timu itakayo msajili.
KAVUMBAGU AANIKA USHIRIKINA SOKA LA BONGO
Title: KAVUMBAGU AANIKA USHIRIKINA SOKA LA BONGO
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Didier Kavumbagu sio jina geni miongoni mwa wadau wa soka nchini kutokana na kuwahi kuzichezea timu za Yanga na Azam FC kwa nyakati tofaut...





Post a Comment