SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: ATLETICO YAITUPA NJE ARSENAL EUROPA, YAINGIA FAINALI
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Atletico Madrid imetinga fainali ya michuano ya Europa baada ya kuifunga Arsenal bao moja katika nusu fainali ya pili uliofanyika katika u...
Atletico Madrid imetinga fainali ya michuano ya Europa baada ya kuifunga Arsenal bao moja katika nusu fainali ya pili uliofanyika katika uwanja wa Wanda Metropolitano.

Vijana hao wa Diego Simeone wameingia hatua hiyo kwa jumla ya mabao 2-1 kufuatia sare ya bao moja katika nusu fainali ya kwanza iliyofanyika uwanja Emirates wiki iliyopita.

Mshambuliaji Diego Costa alifunga bao hilo pekee dakika ya 45 baada ya kupokea pasi ya Antoine Griezmann.

Marseille nayo imeingia hatua hiyo baada ya kuitoa Salzburg kwa jumla ya mabao 3-2.

Katika mchezo huo ulioenda muda wa nyongeza wenyeji Salzburg walipata ushindi wa mabao 2-1.

Mechi ya nusu fainali ya kwanza iliyofanyika nchini Ufaransa, Marseille iliibuka na ushindi wa mabao 2-0

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top