SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: GERRARD MENEJA MPYA RANGERS
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Steven Gerrard ameteuliwa kuwa Meneja mpya wa timu ya Fc Rangers ya Scotland kwa mkataba wa miaka minne. Sky Sports iliripoti mapema kuw...
Steven Gerrard ameteuliwa kuwa Meneja mpya wa timu ya Fc Rangers ya Scotland kwa mkataba wa miaka minne.

Sky Sports iliripoti mapema kuwa Gerrard atapewa kibarua hicho kufuatia mazungumzo yaliyofanyika jijini London jana usiku.

Gerrard, 37 alikuwa kocha wa kituo cha kukuzia vipaji cha Liverpool tangu mwezi Aprili mwaka jana lakini kuanzia msimu ujao atakuwa Meneja.

"Ni heshima kubwa kwangu kuwa Meneja mpya wa Rangers, ninafahamu tamaduni na historia ya klabu hii.

"Nafurahi kuanza safari mpya ya soka hapa Rangers, ninataka kuhakikisha tunaweza kuweka historia mpya ya mafanikio ndani ya klabu hii," alisema Gerrard.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top