SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: MOURINHO AWABWATUKIA NYOTA WAKE KIPIGO CHA BRIGHTON
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Meneja Jose Mourinho amewatupia lawama wachezaji wake kwa kiwango kibovu walicho onyesha katik mchezo waliopteza kwa bao  dhidi ya Brighto...
Meneja Jose Mourinho amewatupia lawama wachezaji wake kwa kiwango kibovu walicho onyesha katik mchezo waliopteza kwa bao  dhidi ya Brighton jana usiku.

Mourinho ameiambia Sky Sports kuwa, "Haikuwa nzuri kwetu, wachezaji waliochukua nafasi wenzao wameshindwa kufanya vizuri.

"Kama mchezaji mmoja mmoja akishindwa kufanya vizuri usitegemee timu kufanya vizuri. Nadhani mtaelewa kwanini baadhi ya wachezaji wanapata nafasi kubwa uwanjani kuliko wengine.
Mourinho aliongeza kuwa, "Siwezi kusema sikufurahi sababu nawafahamu vizuri wachezaji wangu, wale waliokuwa wanasema kwanini kila siku namtumia Romelu  Lukaku watakuwa wamepata jibu.

"Labda hatuna wachezaji wenye uwezo binafsi ndio maana nasema tukimaliza nafasi ya pili itakuwa ni nzuri kwetu.

"Lakini kwa sasa tunahitaji pointi nne ili kuipata nafasi hiyo na tutajitahidi kuzipata," alisema Mourinho.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top