Ndanda ipo nafasi ya pili kutoka chini kwenye msimamo ikiwa
na pointi 23 hivyo kama watapoteza mchezo huo watakuwa kwenye hali mbaya zaidi.
Mchezo huo utakuwa ni wa 27 hivyo itasalia na mechi tatu
ambazo zitaamua kama wanashuka daraja au wanabaki.
Msemaji wa klabu hiyo, Idrissa Bandari amesema wanaiheshimu
Simba kutokana na ubora iliyonayo kwa sasa lakini watapambana kuhakikisha
wanapata pointi tatu ili kujikwamua.
"Tunahitaji sana kupata pointi tatu, hatupo kwenye hali
nzuri, wachezaji wanalijua hilo lakini tunajua Simba ni timu bora ila tutaingia
uwanjani kutafuta pointi tatu," alisema Bandari.
Simba inahitaji pointi tatu ili kujihakikishia kuchukua
ubingwa msimu huu kitu ambacho kinaufanya mchezo huo utakaofanyika uwanja wa
Taifa saa 10 jioni kuwa na ushindani mkubwa.


Post a Comment