Kocha wa zamani wa timu ya Yanga, George Lwandamina amehoji kanuni zilizotumika na kumfungia mlinzi Kelvin Yondani kwa kumtemea mate Asante Kwasi wa Simba katika mechi ya watani wa jadi Aprili 29.
Wiki iliyopita Mtendaji mkuu wa bodi ya ligi, Boniface Wambura alitangaza kumsimamisha mlinzi huyo kutokana na kitengo hicho na kulipeleka suala hilo kwa kamati ya nidhamu ya TFF.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Lwandamina ambaye juzi ametangazwa kuwa kocha mpya wa Zesco United ya Zambia ameshangazwa na tukio hilo kwakua mlinzi huyo alifanyiwa kitendo hicho kwenye mchezo dhidi ya Singida United na hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa.
Lwandamina aliandika hivi, "Sielewi kanuni gani zilitumika kumfungia Kelvin Yondani katika mchezo dhidi ya Simba, kanuni hizo hizo hazikutumika kwenye mechi ya Singida dhidi ya Yanga. Itachukua muda mrefu kwa soka la Tanzania kupiga hatua.
Yondani ndio muhimili mkubwa wa safu ya ulinzi ya Yanga kwa sasa ambapo amechaguliwa nahodha msaidizi wa kikosi hicho.
SAKATA LA KUFUNGIWA YONDANI LAMUIBUA LWANDAMINA
Title: SAKATA LA KUFUNGIWA YONDANI LAMUIBUA LWANDAMINA
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Kocha wa zamani wa timu ya Yanga, George Lwandamina amehoji kanuni zilizotumika na kumfungia mlinzi Kelvin Yondani kwa kumtemea mate Asant...



Post a Comment