Timu ya Yanga imesahau kutolewa kwenye michuano ya FA na wapo kwenye maandalizi ya mechi ya Shirikisho Afrika dhidi ya Wolaita Dicha siku ya Jumamosi.
Yanga ilitupwa nje ya michuano ya FA na Singida United kwa mikwaju ya penati 4-2 Aprili mosi baada ya kutoka sare ya bao moja katika muda wa kawaida.
Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano wa klabu hiyo, Dismas Ten amesema wameuchukulia mchezo huo kwa umuhimu mkubwa na maandalizi yanaendelea vizuri.
Ten amesema wachezaji wapo kambini mkoani Morogoro wakijiandaa wakiwa na morali ya hali juu wakiahidi kufanya vizuri na kumaliza ka
"Kikubwa ninawaomba mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi siku ya Jumamosi kuipa sapoti timu wakiwa na jezi zao za kijani ili kuhakikisha tunashinda hapa nyumbani," alisema Ten.
Katika mchezo huo Yanga itakosa huduma za wachezaji wanne wa kikosi cha kwanza Kelvin Yondani, Papy Tshishimbi, Obrey Chirwa na Said Makapu ambao wana kadi mbili za njano kila mmoja.
YANGA: YALIYOPITA SI NDWELE
Title: YANGA: YALIYOPITA SI NDWELE
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Timu ya Yanga imesahau kutolewa kwenye michuano ya FA na wapo kwenye maandalizi ya mechi ya Shirikisho Afrika dhidi ya Wolaita Dicha siku ...
Post a Comment