SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: AZAM YAKANUSHA KUMTIMUA ABDUL MOHAMMED
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Uongozi wa klabu ya Azam FC umekanusha taarifa zilizozagaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa imemfuta kazi Mkurugenzi wake mkuu Abdul Mohamm...
Uongozi wa klabu ya Azam FC umekanusha taarifa zilizozagaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa imemfuta kazi Mkurugenzi wake mkuu Abdul Mohammed.

Jana jioni kulitoka taarifa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii ikieleza klabu hiyo imemfuta kazi kutokana na mwenendo mbovu wa timu hiyo.

Msemaji wa klabu hiyo, Jaffer Idd amewaambia waandishi wa habari kuwa hajapokea taarifa yoyote kutoka kwenye Menejimenti kuhusu mabadiliko ya kiuongozi.

Jaffer ameongeza kuwa endapo kutakuwa na mabadiliko yoyote yatawekwa wazi na wadau wa soka watapewa taarifa.

"Suala la Mkurugenzi Abdul Mohammed sijaambiwa chochote na Menejimenti kwahiyo siwezi kulisemea kwakua halijaletwa kwangu," alisema Jaffer.

Hata hivyo taarifa ambalo hazikuthibitishwa zinasema kuna kiongozi mwandamizi kutoka TFF anakamilisha utaratibu wa kurithi mikoba yake.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top