Mlinzi wa timu ya Azam FC, Daniel Amoah leo atafanyiwa upasuaji mara mbili ili kutibu majeraha yanayo mkabili katika hospitali ya Vincent Parrot ya Afrika Kusini.
Raia huyo wa Ghana alipelekwa nchini humo wiki iliyopita kwa ajili ya matibabu baada ya kupata majeraha.
Amoah atafanyiwa upasuaji wa goti na wa mfupa wa mguu uliokuwa umechanika hivyo atakaa nje ya uwanja kwa miezi tisa.
Msemaji wa klabu hiyo, Jaffer Idd amesema mlinzi huyo alifanyiwa vipimo juzi na kutakiwa upasuaji ambao utafanyika leo.
"Mchezaji wetu Daniel Amoah ambaye yupo Afrika Kusini atafanyiwa upasuaji leo mara mbili wa goti na mguu uliochanika katika hospitali ya Vincent Parrot hivyo atakuwa nje ya uwanja kwa miezi tisa," alisema Jaffer.
Jaffer alisema mlinzi wao David Mwantika aliyelazwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili kitengo cha moyo cha Jakaya Kikwete anaendelea vizuri naye pia leo atafanyiwa vipimo zaidi.
BEKI WA AZAM KUPASULIWA MARA MBILI LEO
Title: BEKI WA AZAM KUPASULIWA MARA MBILI LEO
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Mlinzi wa timu ya Azam FC, Daniel Amoah leo atafanyiwa upasuaji mara mbili ili kutibu majeraha yanayo mkabili katika hospitali ya Vincent ...
Post a Comment