SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: KUZIONA YANGA, DICHA BUKU TATU
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Uongozi wa klabu ya Yanga umetangaza kiingilio cha chini katika mchezo wake wa kombe la Shirikisho Afrika dhidi Wolaita Dicha ya Ethiopia ...
Uongozi wa klabu ya Yanga umetangaza kiingilio cha chini katika mchezo wake wa kombe la Shirikisho Afrika dhidi Wolaita Dicha ya Ethiopia kitakuwa shilingi elfu tatu (3000).

Yanga itacheza na Dicha, Aprili 7 katika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo ambao watatakiwa kushinda ili kujiweka kwenye mazingira katika mchezo wa marudiano.

Viingilio hivyo vimetangazwa kuwa VIP A ni sh 15,000, VIP B na C sh 10,000 wakati mzunguko utakuwa sh 3000.

Yanga imeweka viingilio hivyo rafiki ili kuwafanya mashabiki wengi kujitokeza kuwapa sapoti wachezaji uwanjani.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top