Timu ya Taifa ya Wanawake ya Tanzania 'Twiga Stars' imeshindwa kutumia vizuri uwanja wa nyumbani baada ya kulazimishwa sare ya mabao 3-3 Zambia 'Shepolopolo' katika mchezo wa kufuzu fainali za Afrika katika mchezo uliofanyika uwanja wa Taifa.
Twiga itatakiwa kushinda au kutoka sare inayoanzia mabao manne ili kufuzu hatua inayofuata.
Mshambuliji nyota wa Twiga Stars Asha Rashid 'Mwalala' alifunga mabao mawili dakika ya 21 na 47 wakati lile la kwanza likifungwa na Stumai Abdallah dakika ya pili tu ya mchezo.
Badra Banda wa Shepolopolo nae alifunga mabao mawili dakika za 25 na 74 huku Musozi Zullu akifunga moja dakika ya 46.
Huu ni muendelezo wa timu za Taifa za Tanzania kushindwa kutumia vizuri uwanja wa nyumbani kwenye michuano ya kimataifa na kushindwa kusonga mbele.
Wiki iliyopita timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 20 'Ngorongoro heroes' ililazimishwa sare na DR Congo kwenye kufuzu michuano ya Afrika vijana.
About Author

Advertisement

Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment