Liverpool imeichakaza Manchester City kwa kuifunga mabao 3-0 katika mchezo wa robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya katika mchezo uliofanyika uwanja wa Anfield.
Kipigo hicho hakikutarajiwa na wengi kutokana na kasi waliyokuwa nayo City iliyo chini ya kocha Pep Guardiola kuruhusu mabao ya haraka kila baada ya dakika 10.
Mohammed Salah aliifungia Liverpool bao la kwanza dakika ya 12 kabla ya Alex Chamberlain kufunga la pili dakika ya 21.
Sadio Mane aliongeza la tatu dakika ya 31 akimalizia mpira wa Salah na kujiweka vizuri kwenye mchezo marudiano utakaopigwa Etihad wiki mbili zijazo.
Katika mchezo mwingine Barcelona imeibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya AS Roma ugenini.
Mabao ya Barcelona yalifungwa na Gerrard Pique na Luis Suarez huku mawili mengine wakijigunga walinzi wa Roma wakati la kufuatia machozi likiwekwa kimiani na Edin Dzeko.
LIVERPOOL YAIPA KIGIPO CHA MSHANGAO MAN CITY ANFILED
Title: LIVERPOOL YAIPA KIGIPO CHA MSHANGAO MAN CITY ANFILED
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Liverpool imeichakaza Manchester City kwa kuifunga mabao 3-0 katika mchezo wa robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya katika mc...
Post a Comment