Uongozi wa timu ya Yanga umekiri kuwakosa wachezaji wanne kuelekea mchezo wa kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Wolaita Dicha siku ya Jumamosi itawapa wakati mgumu.
Yanga itawakosa Papy Tshishimbi, Kelvin Yondani, Obrey Chirwa na Said Makapu kutokana na kuwa kadi mbili za njano.
Katibu mkuu wa klabu hiyo, Boniface Mkwasa amesema kukosekana kwa wachezaji hao ni pengo kutokana na kikosi chao kuandamwa na idadi kubwa ya majeruhi.
Mkwasa amesema benchi la ufundi limeliona jambo hilo na wameandaa kikosi cha wachezaji waliopo ambao wana uwezo pia wakuipa matokeo mazuri timu hiyo.
"Kuwakosa wachezaji hawa ni pengo kubwa lakini waliobaki wanaweza kuziba nafasi zao na kutupa matokeo ya ushindi benchi tayari ufundi limeliona hilo," alisema Mkwasa.
Hata hivyo kurejea kwa nyota Donald Ngoma na Thaban Kamusoko kumeongeza matumaini ya mabingwa hao kufanya vizuri.
TSHISHIMBI NA WENZAKE WAITESA YANGA
Title: TSHISHIMBI NA WENZAKE WAITESA YANGA
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Uongozi wa timu ya Yanga umekiri kuwakosa wachezaji wanne kuelekea mchezo wa kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Wolaita Dicha siku ya Jum...
Post a Comment