Kiungo wa Liverpool Alex Oxlade-Chamberlain amesema ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Manchester City jana ulitokana na sapoti kubwa kutoka kwa mashabiki wao.
Vijana hao wa kocha Jurgen Klopp wana nafasi kubwa ya kutinga nusu fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya baada ya ushindi wa jana.
Liverpool ilipata mabao matatu ndani ya dakika 31 lakini watatakiwa kuyalinda katika mchezo wa maruadiano utakaofanyika uwanja wa Etihad Jumanne ijayo.
Oxlade-Chamberlain, ambaye alifunga bao la pili kwa shuti la mbali lililomshinda mlinda mlango Ederson amekiri kuwa mashabiki wao walifanya kazi kubwa kwenye uwanja wa Anfield.
"Tulikuwa na mwanzo mzuri kabla ya mapumziko na tukapata mabao matatu, uwanja ulijaa na mashabiki walishangilia mwanzo mwisho tangu tunaingia uwanjani kupasha.
"Baada ya kupata mabao matatu kipindi cha kwanza, cha pili tulirudi kwa kuzuia na kufanikiwa kupata ushindi nyumbani ila mashabiki walifanya kazi kubwa," alisema Chamberlain.
Hii ni mara ya pili kwa Muingereza huyo kufunga bao dhidi ya City msimu huu kwa shuti la umbali mrefu kufuatia kufanya hivyo mwezi Januari katika ushindi wa mabao 4-3.
CHAMBERLAIN ATAJA MASHABIKI USHINDI DHIDI YA MAN CITY
Title: CHAMBERLAIN ATAJA MASHABIKI USHINDI DHIDI YA MAN CITY
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Kiungo wa Liverpool Alex Oxlade-Chamberlain amesema ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Manchester City jana ulitokana na sapoti kubwa kutoka kw...
Post a Comment