SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: BOCCO ASISITIZA MSHIKAMANO KWA WANASIMBA
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Nahodha wa timu ya Simba, John Bocco 'Adebayor' amesisitiza mshikamano kwa viongozi, wachezaji, wanachama na mashabiki wa Wekundu ...
Nahodha wa timu ya Simba, John Bocco 'Adebayor' amesisitiza mshikamano kwa viongozi, wachezaji, wanachama na mashabiki wa Wekundu hao ili kutwaa taji la ligi kuu msimu huu.

Bocco alifunga mabao yote mawili katika ushindi wa jana dhidi ya Njombe na kuifanya Simba kujikita kileleni mwa msimamo ikiwa na alama 49 ikiwa juu kwa pointi tatu dhidi ya Yanga.

Mshambuliji huyo alisema licha ya ushindi wa jana lakini ligi bado ni ngumu na mshikamano unahitajika ili kufanikiwa kupata ubingwa msimu huu.

Bocco ameongeza kuwa mbio za ubingwa bado zipo wazi na wao hawawezi kubweteka ambapo wachezaji wapo tayari kujitoa kwa ajili la kukamilisha zoezi hilo.

"Nichukue nafasi hii kuwataka Wanasimba wote kuendelea kushikamana katika kipindi hiki mpaka mwisho wa msimu ili tupate ubingwa," alisema Bocco.

Ili kushiriki michuano ya Afrika mwakani tiketi pekee iliyobaki kwa Simba ni kutwaa taji la ligi baada ya kutolewa mapema katika kombe la Shirikisho.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top