Mchezaji bora wa dunia mara tano, Cristiano Ronaldo ameendelea kudhihirishia ulimwengu kuwa anatisha baada ya kuiwezesha Real Madrid kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Juventus.
Mchezo huo wa robo fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya uliofanyika kwenye uwanja wa Juventus Arena ambapo Ronaldo alifunga mabao mawili na kutengeneza la mwisho.
Ronaldo alifunga bao la kwanza dakika ya tatu baada ya kupokea pasi ya Isco wakati lile la pili akimalizia mpira wa mlinzi Dani Carvajal dakika ya 64.
Mshambuliji nyota wa Juventus, Paulo Dybala alitolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 66 kufuatia kadi ya pili ya njano kutokana na mchezo usio wa kiungwana.
Marcelo aliwafungia mabingwa hao wa kihistoria bao la tatu dakika ya 72 akimalizia pasi ya Ronaldo ambaye alikuwa katika kiwango bora kama kawaida yake.
Mchezo mwingine Bayern Munich imepata ushindi wa mabao 2-1 ugenini dhidi ya Sevilla.
Sevilla walikuwa wa kwanza kupata lililofungwa na Sarabia dakika ya 31 kabla Jesus Navas kujifunga dakika sita baadae huku Thiago Alcantara akiifungia Bayern bao la ushindi dakika 68.
RONALDO HII SASA SIFA! JUVE WAJUTA KUMFAHAMU
Title: RONALDO HII SASA SIFA! JUVE WAJUTA KUMFAHAMU
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Mchezaji bora wa dunia mara tano, Cristiano Ronaldo ameendelea kudhihirishia ulimwengu kuwa anatisha baada ya kuiwezesha Real Madrid kuibu...
Post a Comment