SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: NIYONZIMA, MBONDE WAREJEA SIMBA IKITAKATA MBELE NJOMBE
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Nyota wawili wa timu ya Simba kiungo Haruna Niyonzima na mlinzi Salim Mbonde waliokuwa majeruhi wa muda mrefu wamerejea dimbani wakati Wek...
Nyota wawili wa timu ya Simba kiungo Haruna Niyonzima na mlinzi Salim Mbonde waliokuwa majeruhi wa muda mrefu wamerejea dimbani wakati Wekundu hao wakiibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Njombe Mji.

Mchezo huo wa ligi kuu uliopigwa kwenye uwanja wa Sabasaba mkoani Njombe ilikuwa muhimu kwa timu zote wakati Simba ikitaka pointi tatu ili kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kuchukua ubingwa wakati Njombe wakitaka kujinusuru na janga la kushuka daraja.

Mbonde aliingia dakika ya 56 kuchukua nafasi ya James Kotei aliyeumia wakati Niyonzima akiingia dakika ya 81 kuchukua nafasi ya Shiza Kichuya.

Nahodha John Bocco aliifungia Simba bao la kwanza dakika ya 17 akiwa nje ya 18 baada ya kupokea pasi ndefu kutoka kwa mlinzi Yusuph Mlipili.

Baada ya bao hilo Njombe walifanya mashambulizi ya kutaka kurudisha lakini jitihada zao ziliishia kwa safu ya ulinzi ya Simba iliyokuwa chini ya Juuko Murshid, Erasto Nyoni na Mlipili.

Kipindi cha pili Simba waliongeza kasi na kuliandama lango la Njombe Mji ambapo walifanikiwa kupata bao la pili lililofungwa Bocco tena dakika ya 64 akimalizia krosi ya Shomari Kapombe.

Simba imeendelea kujiimarisha kileleni mwa msimamo ikiwa na pointi 49 alama tatu juu ya watani wao Yanga walio nafasi ya pili huku timu zote zikicheza mechi 21.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top