SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: SHIME AJIGAMBA KUITOA SINGIDA NUSU FAINALI FA
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Kocha mkuu wa timu ya JKT Tanzania, Bakari Shime amejinasibu kuwa kikosi chake kinaweza kuibuka na ushindi mbele ya Singida United kwenye ...
Kocha mkuu wa timu ya JKT Tanzania, Bakari Shime amejinasibu kuwa kikosi chake kinaweza kuibuka na ushindi mbele ya Singida United kwenye mchezo wa nusu fainali ya kombe la FA.

Shime alishuhudia mchezo wa robo fainali kati ya Singida dhidi ya Yanga, Aprili mosi kwenye uwanja wa Namfua na kusema ameona nguva za wapinzani hao pamoja na mapungufu yao.

Shime ameiambia SDF Sports wanafanya maandalizi kabambe kuelekea mchezo huo na kwa jinsi alivyowatazama wapinzani hao anaamini vijana wake wanaweza kupata ushindi na kutinga fainali.

"Tunakwenda kujiandaa na mchezo wetu wa nusu fainali na tayari tushamjua mpinzani wetu, kwa jinsi nilivyowaona nina matuimani ya kuibuka na ushindi," alisema Shime.

JKT ilitinga hatua hiyo baada ya kuitoa Tanzania Prisons kwa kuifunga mabao 2-0 kwenye mchezo wa robo fainali uliofanyika katika uwanja wa Sokoine, Machi 31.

Michezo ya nusu fainali ya michuano ya FA itafanyika Apili 20 na 21 mwaka huu.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top