Licha ya uongozi wa klabu ya Yanga kushindwa kuthibitisha kuwa kocha wao George Lwandamina ametimka na kurejea Zesco United lakini mabingwa hao Zambia wametoa taarifa ya kumalizana na mkufunzi huyo.
Lwandamina alichukua nafasi ya kocha Hans van Pluijm miaka miwili na kuiwezesha Yanga kutwaa ubingwa wa ligi msimu uliopita.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu mkuu wa Zesco, Richard Mulenga imesema tayari wameshamalizana na Lwandamina na atatangazwa muda wowote kutoka sasa.
Hata hivyo uongozi wa Yanga umeshindwa kuthibitisha kuwa kocha huyo ametimka baada ya viongozi wote kushindwa kupokea simu.
Lwandamina aliipa mataji mawili ya ligi kuu nchini Zambia na lile la Barclays kabla ya kujiunga na Zesco.
Inasemakana moja ya sababu iliyosababisha kocha huyo kutimka kwa mabingwa hao watetezi wa ligi ni malimbikizo ya mshahara huku mkataba wake ukimalizika.
YAMETIMIA! LWANDAMINA ATIMKA YANGA
Title: YAMETIMIA! LWANDAMINA ATIMKA YANGA
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Licha ya uongozi wa klabu ya Yanga kushindwa kuthibitisha kuwa kocha wao George Lwandamina ametimka na kurejea Zesco United lakini mabingw...
Post a Comment